Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto – November 2024
Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto – November 2024
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imetangaza nafasi za ajira kwa Watanzania wenye sifa stahiki. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto amepokea kibali kipya cha ajira kwa mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA.170/448/01/“A”/142 cha tarehe 14 Agosti 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi anakaribisha maombi kwa nafasi za kazi zifuatazo:
Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi Nane (08)
1.1 Majukumu ya Kazi
- Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye rejista (Incoming Correspondence Register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (Outgoing Correspondence Register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu/nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filing Cabinets) au sehemu nyingine za kuhifadhi.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya taasisi (File tracking).
1.1.1 Sifa za Mwombaji
- Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Ujuzi wa kutumia kompyuta ni lazima.
1.1.2 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 hadi 45, isipokuwa wale walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha aina ya ulemavu katika mfumo wa kuombea ajira.
- Waombaji waambatanishe CV yenye maelezo binafsi, anuani, namba za simu, barua pepe, na majina ya wadhamini watatu.
- Hati za “Provisional,” “Testimonials,” au “Statement of results” HAZITAKUBALIWA.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliostaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali maalum.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa (Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, na Vyeti vya Kitaaluma).
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
- Taarifa na sifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na iwe na anuani iliyoelekezwa kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto,
Mtaa wa Boma,
S.L.P 98,
27582 Kibaya, Kiteto.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani: https://portal.ajira.go.tz. Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kubofya sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 23 Novemba 2024.
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafikiriwa.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Kwa habari zaidi kuhusu nafasi hizi za kazi na nyinginezo, tembelea habari50.com kwa taarifa za ajira za kila siku.