NAFASI 21 za Kazi Wilaya ya Mwanga July 2024
NAFASI 21 za Kazi Wilaya ya Mwanga July 2024
NAFASI 21 za Kazi Wilaya ya Mwanga July 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 11
MAJUKUMU YA KAZI YA MTENDAJI WA KIJIJI III
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utelekezaji wa Miradi ya Maendeleo
ya Kijiji; - Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuondoa njaa umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji;
- Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko ya migogoro ya Wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji;
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata;
- Pamoja na kazi nyingine atakazopangiwa na Mwajiri wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne au Sita, Astashahada/Cheti NTA/LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 04
MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara / Kitengo/ Sehemu husika,
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka
sehemu zinazohusika; - Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada (Diploma) ya
Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za Kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, internet, email na Pyblisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 05
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Regista (Incomming Correspondence Register);
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
- Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa;
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na
Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka Vyuo
vinavyotambuliwana Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
MUHUDUMU WA JIKONI – NAFASI 01
MAJUKUMU YA KAZI YA MUHUDUMU WA JIKONI
- Kuangalia usafi wa mazingira ya jikoni;
- Kupika vyakula vya aina mbalimbali;
- Kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula ni safi;
- Kuhakikisha usalama wa jiko.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV). Awe na Astashahada (Mafunzo ya mwaka mmoja) katika fani Uhudumu wa jikoni kutoka Vyuo vinavyotambuliwana Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGOS A.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
NACTE). - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 31 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA MWANGA,
S.L.P.716
MWANGA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga More Details |
2024-07-31 Login to Apply |
POST: MHUDUMU WA JIKONI DARAJA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga More Details |
2024-07-31 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga More Details |
2024-07-31 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 11 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga More Details |
2024-07-31 Login to Apply |
Sifa za Habari50.com Habari50.com ni blog maarufu ya habari inayojulikana kwa kutoa taarifa za uhakika na kwa wakati kuhusu matukio mbalimbali nchini Tanzania na kwingineko. Blog hii inajitahidi kuwaletea wasomaji wake habari moto moto na za kina kuhusu masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na michezo. Kwa taarifa zaidi kuhusu ajali hii na habari zingine za kitaifa na kimataifa, tembelea Habari50.com na ujipatie habari za kuaminika na za kina.
Tunatoa pole kwa familia ya marehemu Jumwema Charles na kuwatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa katika ajali hii mbaya. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo kamili cha ajali hii na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuepusha ajali kama hizi kutokea