NACTVET Matokeo ya Uchaguzi wa Awamu ya Pili 2024/2025

Filed in HABARI by on August 21, 2024 0 Comments

NACTVET Matokeo ya Uchaguzi wa Awamu ya Pili 2024/2025

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linafuraha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Matokeo haya yalitangazwa rasmi tarehe 18 Agosti, 2024, na yanapatikana kwa umma kupitia tovuti rasmi ya NACTVET.

NACTVET ilifungua dirisha la awamu ya pili la udahili kuanzia tarehe 11 Julai hadi tarehe 10 Agosti, 2024. Katika kipindi hiki, jumla ya waombaji 20,163 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo na programu walizozipendelea. Hata hivyo, waombaji 3,806 walikosa sifa zinazohitajika kwa programu walizoomba.

Kwa upande mwingine, jumla ya waombaji 13,201 wamechaguliwa kujiunga na vyuo 206 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi. Katika idadi hii, wanawake ni 6,512, wakichangia asilimia 49.3% ya waliochaguliwa, na wanaume ni 6,689, wakichangia asilimia 50.7%. Kati ya waombaji hao, 193 wamechaguliwa katika vyuo 33 vya serikali, na waombaji 13,008 wamechaguliwa katika vyuo 173 visivyo vya serikali.

Kwa waombaji ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba, Baraza linawashauri kuomba kujiunga katika programu na vyuo vyenye nafasi kupitia dirisha la awamu ya tatu. Dirisha hili limefunguliwa tarehe 18 Agosti 2024 na litafungwa tarehe 30 Agosti 2024. Waombaji wanaweza kuangalia matokeo yao na kupata maelezo zaidi kupitia tovuti ya NACTVET kwa kubonyeza CAS Selection 2024.

BONYEZA LINK HAPA KUDOWNLOAD PDF

Kwa taarifa zaidi na habari mpya, tembelea tovuti yetu au jiunge na habari50.com kwa sasisho za haraka. Habari50.com ni chanzo bora cha habari za elimu na fursa za ajira nchini Tanzania.

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *