VIINGILIO Mechi ya Yanga vs Al Hilal Sudan – 26 Novemba 2024

Filed in MICHEZO by on November 16, 2024 0 Comments

VIINGILIO Mechi ya Yanga vs Al Hilal Sudan – 26 Novemba 2024

Klabu ya Young Africans (Yanga) imewatangazia mashabiki wake viingilio vya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Al Hilal ya Sudan, itakayofanyika tarehe 26 Novemba 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo huu utapigwa kuanzia saa 10:00 jioni, na unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania.

VIINGILIO Mechi ya Yanga vs Al Hilal Sudan – 26 Novemba 2024

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, ametangaza viingilio vya mchezo huo huku akiwataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti Yanga katika harakati za kufuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Viingilio vya Mechi ya Yanga vs Al Hilal Sudan

Mashabiki wa soka wataweza kununua tiketi zao kupitia mitandao ya simu pamoja na vituo maalumu vilivyotangazwa, huku viingilio vikiwa kama ifuatavyo:

Kategoria ya Tiketi Bei (Tsh)
VIP A 30,000
VIP B 20,000
VIP C 10,000
Viti vya Machungwa 3,000
Mzunguko 3,000

Tiketi Zapatikana Wapi?

Tiketi za mechi hii zimeanza kuuzwa leo hii, na zinaweza kununuliwa kupitia mitandao ya simu kama M-Pesa, Tigo Pesa, na Airtel Money, pamoja na vituo maalumu vitakavyotangazwa na klabu ya Yanga. Mashabiki wanahimizwa kununua tiketi mapema ili kuepuka foleni na kuhakikisha wanapata nafasi ya kuishuhudia timu yao ikicheza mubashara.

Ushindi Ni Lazima kwa Yanga

Ally Kamwe amesisitiza kuwa Yanga inahitaji sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wake ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Al Hilal. Amesema kuwa Yanga haijawahi kupoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano yoyote, na hivyo mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuipa hamasa timu yao.

“Hii ni mechi ya kila Mwananchi kujitokeza kuongeza nguvu katika kuhakikisha ushindi unapatikana,” alisema Kamwe.

Kwa mashabiki wa Yanga, hii ni nafasi muhimu ya kuonyesha mapenzi yao kwa timu na kuwaunga mkono wachezaji ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika hatua hii ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *